Jumatano, 9 Desemba 2015

Magufuli aongoza Watanzania kufanya usafi


 Raia nchini Tanzania wameungana na maafisa wa serikali kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi.
Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi.
Mwandishi wa BBC Sammy Awami aliwapata wachuuzi na maafisa wa baraza la jiji Dar es Salaam asubuhi na mapema wakifanya usafi katika soko maarufu la Kariakoo.
Wengi wamefurahia agizo la Rais.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo.
Rais John Magufuli alikuwa kwenye eneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu.
Katika eneo la Mwenge, wananchi pia wanajizatiti kufanya usafi. Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amewapata wananchi hawa wakiteketeza takataka baada ya kuzikusanya pamoja.Alipokuwa akitangaza kubadilishwa kwa utaratibu wa kusherehekea Siku ya Uhuru mwaka huu, Rais Magufuli alisema hatua hiyo italiokolea taifa pesa nyingi ambazo hutumiwa katika maandalizi na kufanikisha sherehe hizo.
“Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Magufuli aongoza Watanzania kufanya usafi Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top