Jumanne, 23 Juni 2015

TAIFA STARS YA BAADAYE YAINGIA KAMBINI

Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania, imeingia kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya jumapili.
Kikosi hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.
U15 ni mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu ka fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar, ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: TAIFA STARS YA BAADAYE YAINGIA KAMBINI Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top