ERASTO EDWARD NYONI NDIYE 'KINGUNGE' WA TAIFA STARS
Erasto Edward Nyoni ndiye mchezaji wa muda mrefu zaidi kwenye kikosi cha kwanza timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Nyota huyo mpole na mwenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya Uwanja, alianza kucheza kikosi cha kwanza Taifa Stars tangu mwaka 2007 chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo na ameendelea kuwamo kikosi cha kwanza hata kwa makocha waliofuatia Wadenmark, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Mholanzi Mart Nooij Poulsen. Je, mbele ya Charles Boniface Mkwasa mchezaji huyo kiraka ataendelea kutamba Taifa Stars?
0 maoni:
Chapisha Maoni