Mubarak:Raia waandamana Misri
Vikosi vya usalama nchini Misri
vimepambana na karibu waandamanaji 2000 karibu na eneo la Tahrir Square
mjini Cairo ambapo mtu mmoja aliuawa.
Maandamano hayo yanafanyika
kufuatia uamuzi wa mahakama wa kumuondolea mashtaka aliyekuwa rais wa
Misri Honi Mubarak kuhusiana na mauaji ya zaidi ya waandamanaji 200
wakati wa maandamano ya mwaka 2011.Kweye mahojiano na kituo kimoja cha runinga baada ya hukumu hiyo bwana Mubarak alisema kuwa hajafanya lolote baya Awali alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini hukumu hyo ikabatilishwa .
Hata hivyo bado yuko kuzuizini baada ya kupatikana na makosa ya ufujaji wa pesa za umma.
0 maoni:
Chapisha Maoni