Jumamosi, 8 Novemba 2014

COSATU yaitoa NUMSA

COSATU yaitoa NUMSA

Jumuia ya wafanyakazi wa Afrika Kusini, COSATU, imekitoa katika jumuia chama cha wachimba migodi, NUMSA - chama kikubwa kabisa na chenye malalamiko mengi ya kisiasa katika jumuia hiyo.
COSATU imchukua hatua hiyo baada ya NUMSA kulalamika dhidi ya Rais Jacob Zuma, na kukataa kuunga mkono chama tawala cha ANC katika uchaguzi wa awali mwaka huu.
NUMSA ilimshutumu Rais Zuma kwamba haungi mkono tena masilahi ya wafanyakazi na kusema kuwa itaanzisha vuguvugu jipya la kishosalisti.
Kiongozi wa NUMSA, Irvin Jim, alisema kuwa COSATU - ambayo zamani ikiwatikisa mabosi wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi - sasa imepooza.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: COSATU yaitoa NUMSA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top