Messi matatani kwa kukwepa kodi
Nyota wa timu ya Barcelona na
Argentina Lionel Messi anakabiliwa na mashtaka ya ukwepaji wa kodi,hii
ni kwa mujibu wa jaji mmoja wa Uhispania.
Jaji huyo amepinga ombi
la kiongozi wa mashtaka la kufutilia mbali mashtaka hayo kwa madai
kwamba babake mchezaji huyo ndiye anayesimamia fedha zake.Messi na babaake Jorge wanashtakiwa kwa kuiibia mamlaka ya taifa hilo zaidi ya yuro millioni 4.
Wote wamekana kufanya makosa hayo yalioanza mwaka 2007.
0 maoni:
Chapisha Maoni