Jumamosi, 4 Oktoba 2014

Ebola yaathiri siku kuu ya Eid

    Ebola yaathiri siku kuu ya Eid

Ripoti kutoka Magharibi mwa Afrika zinasema kuwa sherehe za Eid Ul Adhaa zimeathiriwa vibaya na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Nchini Guinea maeneo ya uma ambapo watu hukongamana ili kufanya ibada yalikuwa bila watu.
Nchini Sierra Leone Muungano wa baraza la maimamu uliwaonya waislamu kutoamkuana kwa kushikana mikono wala kukumbatiana.
Madaktari nchini Ujerumani wanasema kuwa mwanasayansi aliyeambukizwa ugonjwa wa ebola wakati alipokuwa akilifanyia kazi shirika la afya duniani ameponea.
Vilevile Muunguzi wa Ufaransa aliyeambukizwa ugonjwa huo alipokuwa akijitolea katika shirika la madaktari wasio kuwa na mipaka MSF nchini Liberia pia ameponea.
Takriban watu 3400 wamefariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Ebola yaathiri siku kuu ya Eid Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top