Jumapili, 21 Septemba 2014

Wakenya waadhimisha tukio la kigaidi.

Wakenya waadhimisha tukio la kigaidi.

Sherehe tofauti zinafanyika nchini Kenya ili kuadhimisha mwaka mmoja tangu shambulizi la kigaidi la maduka ya West Gate,ambapo takriban watu 67 walipoteza maisha yao ikiwemo washukiwa wanne wa shambulizi hilo.
Kanda ya video ya CCTV kuhusu shambulizi hilo inaonyesha wateja wa duka hilo walioshtuka wakiwatoroka majambazi hao huku wengine wakijificha chini ya meza za maduka yao.
Kundi la wapiganaji wa Alshabaab lilikiri kutekeleza shambulizi hilo.
Siku ya jumamosi ,mkuu wa polisi nchini Kenya alitoa wito kwa raia kuwa macho ili kuepuka shambulizi lolote la kigaidi linalolenga kuambatana na maadhamisho hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Wakenya waadhimisha tukio la kigaidi. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top