NDANDA FC WA BIN SLUM WAANZIA KILELENI LIGI KUU BARA, WATISHIA AMANI AZAM FC
WAGENI
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ndanda FC wameanzia kileleni
kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Stand United Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga.
Maana
yake, Ndanda wanaodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum pamoja na Mbeya City
na Stand United, wanakuwa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa wastani wa
mabao, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC walioshina 3-1 dhidi
ya wageni wengine kwenye ligi hiyo, Polisi Morogoro.
Mtibwa
Sugar iliyoifunga mabao 2-0 Yanga SC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ipo
nafasi ya tatu sawa na Prisons ya Mbeya iliyowachapa wenyeji Ruvu
Shooting mabao 2-0, wakati JKT Mgambo 1-0 iliyoilaza Kagera Sugar 1-0
ipo chini yao.
Mbeya
City iliyolazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine, Mbeya
iko juu ya Yanga SC iliyolala 2-0 na timu nyingine zote zilizopoteza
mechi leo.
Ligi
Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Coastal Union ya Tanga
dhidi ya wenyeji Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Udhamini mnono
na ushindi; Mkurugenzi wa kampuni ya Bin Slum, Nassor Bin Slum kulia
akimkabidhi vifaa kiongozi wa Ndanda kushoto wakati wa kutangaza
kuidhamini timu hiyo mpya ya Ligi Kuu
0 maoni:
Chapisha Maoni