Alhamisi, 25 Septemba 2014

Mahakama ya Kisutu yawaacha wafuasi wa Chadema

Mahakama ya Kisutu yawaacha wafuasi wa Chadema

 Mmoja wa wanachama wa Chadema, Kamugisha Ngaiza, alivyowekwa chini ya ulinzi na polisi hivi karibuni.
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewaachia huru kwa dhamana washitakiwa watatu wenye kesi namba173 ya mwaka 2014, kwa kosa la kumsindikiza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Makao Mkuu ya Polisi.
Washitakiwa hao ni Ngaiza Kamugisha ambaye ni mfuasi wa chama hicho, Katibu wa BAVICHA Temeke, Benito Mwapinga na Elisante Bagenyi ambae ni mfuasi wa chama hicho, walifikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa dhamana kufuatia maombi yaliyopelekwa na wakili wao John Mallya.
Akisoma mashitaka hayo, mbele ya Hakimu mkazi Frenk Moshi, Wakili wa serikali Benard Kongola alidai kuwa mshitakiwa huyo namba moja mwenye miaka (28), mkazi wa Vingunguti alikuwa anakabiliwa na kosa la kutoa lugha chafu na kukiuka amri za jeshi hilo alipokuwa makao makuu.
Alisema kufuatia maombi hayo, washitakiwa wengine wawili ambao walitenda kosa hilo hilo nao waliachiwa juzi kwa dhamana ya sh. mil.5 kwa kila mmoja, huku mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Kamugisha alirudishwa rumande na kutolewa jana kwa dhamana ya kiasi hicho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Mahakama ya Kisutu yawaacha wafuasi wa Chadema Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top