HALMASHAURI YA SINGIDA KUWEKA TARATIBU NA SHERIA ZITAKAZOHIMIZA WANANCHI KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone,akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC), Kulia ni katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan.Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Singida walioshiriki Kikao kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini singida.Picha zote na Nathaniel Limu.
IMEELEZWA
kwamba halmashauri ya wilaya ya Singida,imeshindwa kufikia malengo yake
ya ukusanyaji wa mapato ya ndani,kwa kile kilichodaiwa kuwa wananchi wa
jimbo la Singida mashariki,kuzuiwa kuchangia maendeleo yao.
Hayo
yamesemwa juzi na mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Illuminata
Mwenda,wakati akitoa taarifa yake ya kushindwa kukusanya mapato ndani
kama inavyokusudiwa, kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC)
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini
Singida.
Alisema
wananchi wa jimbo hilo,wamezuiwa kuchangia na kutekeleza miradi yao ya
maendeleo na pia wasilipe ushuru wala kodi kama inavyoelekezwa na
sheria ndogo za halmashauri hiyo.
Mwenda
alisema siasa za aina hiyo,zimechangia ukusanyaji wa mapato ya ndani
kuwa mgumu mno na vile vile zimedumaza maendeleo kwa ujumla katika jimbo
hilo.
Hata
hivyo, mkurugenzi huyo alisema wanaangalia utaratibu wa kisheria
utakaosaidia kuwahimiza wananchi wa jimbo hilo kushiriki kuchangia na
kutekeleza miradi yao ya maendeleo, kama ambavyo wananchi wengine wa
majimbo mengine ya halmashauri,wanavyochangia.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Mkalama,Mussa Chang’a alisema serikali ya
mkoa isiruhusu siasa uchwara kuendelea kwa vile zitapunguza kasi ya
kuwaletea wananchi maendekeo endelevu.
“Ni
afadhali kulaumiwa kuliko kuacha wanasiasa uchwara wanaharibu au
wanadumaza maendeleo ya wananchi, yaliyofikiwa na yanayotarajiwa
kufikiwa”,alisema.
Taarifa
iliyotolewa kwenye kikao hicho, ni kwamba halmashauri ya wilaya ya
Singida ni ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kipindi
cha kuanzia julai mwaka jana hadi machi mwaka huu.
Halmashauri hiyo, imekusanya asilimia 18.4 tu,wakati manispaa ya Singida,imekusanya asilimia 37,Iramba 71.4 na Manyoni 54.
Mbunge
wa jimbo la Singida mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu, ameapa kwamba
wananchi wa jimbo lake watakuwa kwenye likizo ya kuchangia maendeleo
yao,hadi hapo ubunge wake utakapokoma.
0 maoni:
Chapisha Maoni