Diamond ashindwa kutokea kwenye show London, mashabiki wamngonja hadi saa 10 alfajiri, amtupia lawama promota
Kwa mara nyingine tena, mashabiki wa Diamond Platnumz wameshindwa kumuona akitumbuiza licha ya kumsubiria hadi saa 10 Alfajiri.Awamu hii imetokea jijini London, Uingereza katika show aliyoitangaza kwa kiasi kikubwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Tofauti na Stuttgurt, Ujerumani ambako mashabiki walifanya uharibifu mkubwa, mashabiki wa London waliamua kuwa wapole tu na kurejea majumbani mwao na hasira walizozimeza vifuani.
saeedderby: I
was there brov it was maad trust me, even police got involved with that
shit, they had to calm people down untill seven in the morning, people
wanted their money back he I’ll pay the price cause he got arrested
Chanzo
cha Diamond kutotumbuiza kwenye show hiyo kinaonekana kuwa ni kile kile
kama cha Ujerumani wiki kadhaa zilizopita yaani promota kushindwa
kumlipa fedha yake. Staa huyo hakuchelewa kumtupia lawama promota wa
show hiyo, DJ Rule. Akiweka picha ya promota huyo kwenye Instagram,
Diamond ameandika:
Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!….kuweni makini sana na promoter
huyu (Victor – Dj rule) mnaposikia kaandaa show, party au hafla
yoyote…ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwasababu ni tapeli….
si unajua aisifiae mvua imemnyeshea… basi mie nimeloa kabisa.”
0 maoni:
Chapisha Maoni