CHAPANGA KUANDAMANA KESHO
MWENYEKITI WA CHDEMA KHAMA JUMA PROTAS.
Wakati jeshi la Polisi Nchini likipinga maandamano yoyote, Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Kimetangaza kufanya maandamano ya amani kupinga kuendelea kwa bunge la
Katiba.Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Chama hicho
wilayani Humo Juma Protas amesema maandamano hayo yatafanyika kesho
mwaka huu kuanzia asubuhi kwa kushirikisha wanachana na wananchi wengine
wanaounga mkono jambo hilo. Protas amesema maandamano hayo yataanzia
katika ofisi ya Chama hicho, na watazunguka katika mitaa mbalimbali ya
mji wa Kahama na kuhitimisha kwa mkuu wa wilaya ya Kahama na kwamba
lengo kuu ni kuitaka serikali kusitisha bunge la katiba.
Amesema katiba Mpya kwa vyovyote haiwezi kupatikana kwa mwaka huu
hivyo kuendelea kwa bunge la katiba ni kutumia vibaya fedha za wananchi
na kwamba wanatumia sheria ya maandamano ya kimataifa kwa kufunga
kitambaa cheupe mkononi kuashiria amani.
Protas amesema kwa upande wa Halmashauri ya Msalala, chama hicho
kitafanya maandamano siku hiyohiyo kuanzia ofisi za Chadema-Segese na
kuzunguka Mitaani na kuhitimisha katika uwanja wa shule ya msingi Segese
kwa kuzungumza na wananchi.
Hata hivyo amesema licha ya kuomba Kibali kwa Jeshi la Polisi wilaya
ya Kahama, hakuna majibu waliyopewa na jeshi hilo, huku mwenyekiti huyo
akisisitiza watatumia kuwa sheria ya kimataifa kufanya maandamano bila
kuathiri kitu chochote.
0 maoni:
Chapisha Maoni