Jumapili, 7 Septemba 2014

ANGALIA PICHA MSAFARA WA MAALIM SEIF WAPATA AJALI

 Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi.  Habari zinasema msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi umepata ajali ukihusisha magari mawili ya msafara wa kiongozi huyo ambayo jumla yake yalikuwa saba yalipogongana na lori lenye tela. 

Akizungumza na mtandao huu, Mkurughenzi wa Habari wa CUf, Adam Kambaya alisema  Viongozi wawili wa CUF, katibu wa wilaya ya Nyamagana na mwenyekiti wa mtaa wa Nyamagana  ambao hakuwataja majina wamelazwa katika Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.





 Keria ya moja ya magari yaliyopata ajali ikiwa chini baada ya kufyatuka baada ya ajali.
 Hili ni gari lingine ambalo lenye usajili namba T397ANU nalo lilihusika katika ajali hiyo leo.  

 Katibu wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mwenda amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando (kulia) na muonekano wa gari (kushoto) baada ya ajali katika wilaya ya Misungwi, jijini Mwanza.  
Mkuu wa kitengo cha habari Wilaya, Mh Shido ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtaa Utemini Kata ya Mirongo amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top