Jaji Werema awataka wajumbe walio nje ya Bunge Maalum kurejea bungeni
Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.
Jaji Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge hilo.
Jaji Werema amesema wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kupata katiba bora kwa nchi na watu wake.
Aidha, Jaji Werema ameviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa
na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi
kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni