Wachezaji wa Ghana walipwa fedha zao
Serikali ya Ghana imetuma dola millioni 3 nchini
Brazil ili kuwalipa wachezaji wake wa soka fedha za kushiriki katika
michuano hiyo wanazodai.
Naibu Spika Joseph Yamin ameiambia radio ya Citi
Fm nchini humo kwamba,''wachezaji wamesisitiza kwamba ni sharti wapewe
fedha hizo taslimu .Ghana ni sharti iishinde Ureno siku ya alhamisi ili kujikatia tiketi ya kuendelea kushiriki katika michuano hiyo.
Iwapo itashindwa ama kutoka sare yoyote basi itakuwa imebanduliwa katika mashindano hayo,na iwapo watashinda na Ujerumani na Marekani kutoka sare katika mechi nyengine ya kundi G basi watakuwa wametolewa.
Mapema juma hili kulikuwa na madai kwamba timu hiyo ya Black Stars ilikuwa ikipanga kugoma iwapo hawatalipwa fedha hizo.
Na huku wasiwasi ukiendelea katika kambi ya timu hiyo ,rais wa Ghana John Dramani Mahama yeye mwenyewe aliingilia kati na kuwaahidi wachezaji hao kwamba watalipwa fedha zao.
Taarifa kutoka shirikisho la soka la Ghana ilisema;''Serikali inawalipa wachezaji wa timu hiyo fedha za kushiriki katika michuano ya kombe la dunia na fedha hizo zitarudishwa wakati shirikisho la soka duniani FIFA litakapolipa fedha za kushiriki katika mechi hizo baada ya kukamilika kwa michuano hiyo''.
FIFA:Suarez akabiliwa na marufuku
Mshambuliaji matata wa timu ya
soka ya Uruguay Luis Suarez anakabiliwa na marufuku ya mda mrefu
itakayomlazimu kukosa mechi nyengine za michuano ya kombe la dunia iwapo
atapatikana na hatia ya kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.
Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha
harakati za kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila
dhidi ya Italy siku ya Jumanne.
0 maoni:
Chapisha Maoni