Jumapili, 13 Aprili 2014

           Taifa Stars mpya ya Tukuyu

YEYOTE aliyefika kwenye kambi ya Taifa Stars iliyoko Tukuyu kwenye Makao Makuu ya Wilaya ya Rungwe, Mbeya atakiri kuna kila dalili njema za mafanikio ya soka la Tanzania.
Ukweli ni kwamba, kambi hiyo yenye jumla ya wachezaji 33 walioibuliwa kupitia mpango maalum wa kung’amua wachezaji wenye vipaji kwa ajili ya kuiboresha Taifa Stars inaendeshwa kitaalam na imewekwa mahali sahihi.
Kwa kuwa, Watanzania wengi wanapenda kujua undani wa timu hiyo, hivi karibuni Mwanaspoti lilisafiri hadi Tukuyu na kujionea jinsi kambi hiyo iliyopo kwenye Hoteli ya Land Mark inavyoendeshwa.
Ratiba ya mazoezi
Timu hiyo inafanya mazoezi mara mbili kwa siku, yaani asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu Tukuyu na siku zilizopangwa ni kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi, Jumapili ni siku ya mapumziko.
Mazoezi ya timu hiyo huanza saa 1:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi, lakini kabla ya mazoezi  bendera ya taifa hupandishwa sambamba na wachezaji na viongozi kuimba wimbo wa taifa.
Baada ya mazoezi kumalizika, timu hurejea kambini ambako wachezaji na viongozi hupata kifungua kinywa na muda uliotengwa ni saa moja.
Baada ya kunywa chai, wachezaji hupewa muda wa kupumzika katika vyumba vyao huku wakisubiri chakula cha mchana saa 7:00.
Baada ya chakula cha mchana wachezaji hupewa tena muda wa kupumzika hadi ya saa 9:00 Alasiri ambapo hupewa chai kisha 9:30 hurudi mazoezini yanayoanza saa 10:00 jioni na kumalizika saa 12:OO.
Baada ya mazoezi, bendera ya taifa huteremshwa, kisha timu hurejea kambini, saa 1:30 usiku wachezaji hula chakula cha usiku kisha hupewa muda wa kupumzika hadi saa 3:0O usiku ambapo wote hutakiwa kuwepo vyumbani mwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top