ALI KIBA KUTISHIWA KUUAWA KWA BASTOLA, DIAMOND KUHOJIWA POLISI..!
Ally Saleh ‘Ali Kiba’.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu katika jeshi hilo jijini Dar, Diamond ambaye
amekuwa akitajwa sana katika sakata hilo kupitia mitandao ya kijamii
ataitwa kuhojiwa.
“Unajua
ile kesi ipo hapa Central, awali ilitokea Polisi Msimbazi, sasa
mpelelezi wake amekuwa akifikiria kumwita Diamond ili amhoji maana
anatajwa sana,” kilisema chanzo hicho.
Hivi
karibuni, Ali Kiba alivamiwa usiku na watu zaidi ya watano nyumbani
kwao, Kariakoo jijini Dar ambapo waliruka ukuta na kuingia ndani huku
kila mmoja akiwa na bastola.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Ilidaiwa
kuwa, mmoja kati ya watu hao ambao ilisemekana walitumwa kumuua msanii
huyo, aliibua mzozo wa makusudi kwa wenzake ili kumpa mwanya Kiba
kutoroka kwa vile hakufurahishwa na kitendo hicho.
Habari
zinasema walipoingia ndani huku kelele za mbwa zikasaidia kumshtua staa
huyo, ule mzozo ulioanzishwa na wavamizi hao ulimsaidia Kiba kutoroka
ingawa walimkosakosa risasi.
Ikasemekana
baada ya msanii huyo kukimbia, jamaa ambaye alimkingia kifua alimpigia
simu na kumfungukia watu waliohusika huku ikidaiwa kuwa baadhi yao ni
mastaa wenzake.
“Alinitajia
tu majina lakini nilishindwa kuthibitisha moja kwa moja hivyo
nikayafikisha Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kwa ajili ya uchunguzi,”
alisema Ali Kiba huku akikataa kutaja hata jina moja.
Hata
hivyo, mengine yaliibuka hasa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, miongoni
mwa wasanii waliohusika katika tukio hilo eti ni na Diamond.
Amani
lilimsaka afande mmoja ambaye anajua mwenendo wa kesi hiyo ambaye
alikiri kesi hiyo kuwepo Central lakini alisema mambo yote ni siri ya
kazi.
“Nani atahojiwa, nani hatahojiwa ni siri ya kazi yetu,” alisema.
Juzi, paparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Wimbo wa Number One ili kusikia anazungumziaje manenomaneno hayo ya kwenye mitandao na vinywa vya watu.
Juzi, paparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Wimbo wa Number One ili kusikia anazungumziaje manenomaneno hayo ya kwenye mitandao na vinywa vya watu.
“Nimeshasikia
nikitajwa katika hilo, kimsingi ni madai mazito lakini mimi nipo tayari
kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake kwani najua si kweli na sijui
lolote,” alisema Diamond.
Akandelea: “Mimi na Kiba kuna ugomvi gani hadi nifikie hatua hiyo. Kwanza sina moyo wala uwezo wa kufanya hivyo.”
0 maoni:
Chapisha Maoni