Jumamosi, 21 Desemba 2013

              ZITTO KABWE APOKELEWA KIGOMA KAMA LULU

Sehemu ya Umati wa maelfu ya wananchi na mashabiki wa chama cha demokrasia na maendeleo wakimsikiliza mbunge wa \kigoma kaskazini aliyefutwa uongozi ndani ya CHADEMA. 


Siku chache baada ya Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Dr. Wilbroad Slaa kufanya ziara iliyokumbwa na vikwazo vya kutokukubalika kwa wananchi, fujo, maandamano, mabango na kurushiwa mawe akipingwa  kutokana na kamati kuu ya chama hicho kumfukuza uongozi Zito kabwe, hali imekuwa kinyume kwa mbunge huyo anapoingia mkoani kigoma

Hayo yametokea leo ambapo magari, pikipiki, umati mkubwa wa watu wakubwa kwa wadogo wakiandamana kutoka uwanja wa ndege wa kigoma hadi viwanja vya mwanga centre ambapo amehutubia na kusikilizwa kwa utulivu mkubwa

Kesho Kabwe atazuru wilaya ya kasulu ambako Dr. Slaa alipigwa mawe na kuzomewa na hatimaye kushindwa kuhutubia wananchi baada ya gharika la mawe lililofuatwa na jeshi la polisi kurusha mabomu ya kutoa machozi na mkutano kuvunjika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top