Ijumaa, 29 Novemba 2013

CHUJI APAGAWA NA MAKINDA STARS, ASEMA WADOGO WA UMRI MAMBO MAKUBWA

 Watoto wanajua sana, hadi raha. Hata kucheza nao unafurahi yaani. Mimi nakuambia hii timu ni bora sana iliyokuja huku (CECAFA Challenge), na nina matumaini tutafanya vizuri,”alisema kiungo huyo wa Yanga SC.

Chipukizi waliojumuishwa kikosi cha Stars ni Himid Mao, Michael Pius, Ismail Gambo ‘Kussi’, Hassan Dilunga, Elias Maguri, Joseph Kimwaga, Farid Mussa, Juma Luizio, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Haroun Chanongo.  

Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi.

NGASSA: NIMEKUJA KUWASHIKA NAIROBI

 Akizungumza   Ngassa alisema kwamba ameamua Challenge ya mwaka huu afanye kazi kweli ili kujenga heshima yake binafsi na kuisaidia timu.
“Sikuja kutania hapa, najua haya mashindano ni magumu, lakini ninataka kufanya kazi, na nitafanya. Watanzania tu waniombbe dua ya uzima na nini, baada ya hapo wataona wenyewe,”alisema.

Ngassa ameelezea kundi lao na kusema kwamba kuna upinzani mkali baina ya Burundi, Zambia na wao wakati Somalia amewashusha thamani akisema; wasindikizaji hao”.

Hapa ushindani ni kati yetu na Zambia na Burundi, lakini Somalia kwa kweli sijui kama watafika popote,”alisema Ngassa.   

Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi.

        

PONDAMALI: IVO NDIYE TANZANIA ONE KIHALALI

 
 Juma Pondamali akipanga koni jana Uwanja wa Chuo Kikuu cha Strathmore tayari kuwanoa makip wake na chini ni Ivo Mapunda


YONDAN: ROBO FAINALI KAMA ‘KUMSUKUMA MLEVI’ 

 

 Tuna timu nzuri, nimeona mazoezi yetu kwa kweli yanakwenda vizuri. Mfano pale nyuma mimi ni Morad (Said) wote mabeki wazuri na tutaunda ukuta mzuri, viungo na washambuliaji wote safi  kwa kweli tuko vizuri,”alisema.
Yondan alisema timu yao itaongezeka makali washambuliaji wawili wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu watakapowasili.
Wachezaji hao wanasubiri kuichezea klabu yao, Mazembe Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sfaxien ya Tunisia Novemba 30 mjini Lubumbashi na Desemba 1 watawasili mjini hapa. 
Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi.  
      

KIM ASEMA SASA KAZI NDIYO INAANZA STARS

 Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mechi, Poulsen alisema mchezo wa jana ulikuwa mkali na ulizikutanisha timu nzuri.  

Kipindi cha kwanza tulicheza mchezo tofauti. Tulitumia sana mipira mirefu na ya juu, ambayo siyo staili yetu ya uchezaji.
“Tulibadilika kipindi cha pili na kuwa bora, tuliwashambulia sana Zambia, tulitengeneza nafasi na kupata bao la kusawazisha. Mrisho Ngassa akakosa bao la wazi sana,”alisema Kim.

Hata hivyo, Kim alisema kwamba baada ya mchezo wa jana anakwenda kufanyia kazi mapungufu ili waweze kushinda mechi zijazo dhidi ya Burundi na Somalia. 

SURE BOY AWA MCHEZAJI BORA CHALLENGE  

KIUNGO wa Tanzania Bara Kilimanjaro Stars, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ jana alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi kati ya timu hiyo na Zambia Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos, Kenya.
 

Katika mchezo huo wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Bara na Zambia zilitoka sare ya 1-1 na Sure Boy kwa kuwa Mchezaji Bora atazawadiwa kifurushi kutoka Serikali ya Kenya na king’amuzi kutoka DSTV

Akizungumza baada ya mchezo huo, kiungo huyo wa Azam FC alisema kwamba mvua iliyonyesha kipindi cha kwanza ilimfanya ashindwe kucheza vizuri mwanzoni, lakini hali ilipobadilika kipindi cha pili akaonyesha uwezo wake.

Kwa kweli mvua ilituathiri sana kipindi cha kwanza tukashindwa kucheza, ilituharibia mipango yetu ya michezo kabisa,”alisema mtoto huyo wa winga wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’. 

Pamoja na hayo, Sure amesema anashukuru japo wamepambana kipindi cha pili na kusawazisha bao hadi kupata sare na kwamba mechi zijazo watajitahidi kushinda dhidi ya Burundi na Somalia.

Baada ya mechi za jana za Kundi B, Burundi inapanda kileleni kutokana na ushindi wake wa 2-0 dhidi ya Somalia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top