RICHARD RUKAMBURA AFUNGIWA MIAKA 20,SHAFFIH DAUDA NA WILFRED
KIDAU KILA MMOJA APIGWA FAINI YA MILIONI MOJA.
Wilfred Kidau (nyuma ) na Shaffih Dauda
Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewaadhibu walalamikiwa watano kati ya saba baada ya kufanya mapitio (revision) kwa uamuzi wa Kamati ya Maadili kutokana na maombi ya Sekretarieti, huku Richard Julius Rukambura akifungiwa miaka 20 kujihusisha na mpira wa miguu.
Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewaadhibu walalamikiwa watano kati ya saba baada ya kufanya mapitio (revision) kwa uamuzi wa Kamati ya Maadili kutokana na maombi ya Sekretarieti, huku Richard Julius Rukambura akifungiwa miaka 20 kujihusisha na mpira wa miguu.
Sekretarieti ya TFF iliwasilisha maombi ya mapitio kwa Kamati ya
Rufani ya Maadili ili kupata mwongozo kwa vile kulikuwapo mkanganyiko kwenye
uamuzi wa Kamati ya Maadili, hivyo kuiwia vigumu kwake kuutekeleza.
Uamuzi huo wa mapitio umesomwa leo jioni (Oktoba 15 mwaka huu)
mbele ya waandishi wa habari na wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Makamu
Mwenyekiti Victoria Makani.
Rukambura amefungiwa miaka 20 baada ya kupeleka masuala ya mpira
wa miguu katika mahakama za kawaida kinyume na Ibara ya 75 ya Katiba ya TFF na
kifungu cha 73(3)(b) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013. Adhabu yake
itamalizika Oktoba 15, 2033.
Kabla ya kutoa adhabu hiyo, Kamati imejiridhisha kuwa Rukambura
ni mwanafamilia wa TFF kwa vile aliwahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Pamba ya
Mwanza, na fomu zake za kuomba uongozi TFF ziliidhinishwa na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Shinyanga. Vilevile ni ‘Leadership Aspirant’ kwa mujibu wa
kifungu cha 2(v) cha Kanuni za Utii za TFF toleo la 2013.
Pia imesema kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kusajili
Katiba ya TFF inayokataza masuala ya mpira wa miguu kwenda katika mahakama za
kawaida, na kutaja vyombo vya haki vitakavyoshughulikia masuala hayo (judicial
organs), Kamati ya Maadili ilikosea kutomtia hatiani mlalamikiwa kwa kuegemea
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naye Shaffih Dauda, Kamati imebaini kuwa mwanafamilia wa TFF
kwani ni Mwenyekiti wa Bombom FC, fomu yake ya kuomba uongozi ilipitishwa na
klabu ya Simba na pia ameshakuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya
Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA), hivyo yeye ni ‘Leadership
Aspirant’ kwa mujibu wa kifungu cha 2(v) cha Kanuni za Utii za TFF toleo la
2013.
Hivyo Dauda amepatikana na kosa la kimaadili kwa kutotekeleza
maagizo rasmi ya TFF ya kutosambaza barua iliyotoka Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
Kamati ya Rufani ya Maadili imempa onyo kali na faini ya sh.
milioni moja anayotakiwa kuilipa ndani ya siku tatu ambapo akishindwa kufanya
hivyo atafungiwa mwaka mmoja. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha
6(1)(a),(c) na (h) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
Akilipa faini ataweza kuendelea na mchakato wa kugombea nafasi
ya uongozi aliyoomba.
Nazarius Kilungeja amepatikana na kosa la kimaadili kwa mujibu
wa kifungu cha 73(8)(a) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013, kwani
akijua kuwa ana adhabu ya kinidhamu ya kufungia miaka mitano na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) iliyoanza 2009 alichukua fomu kuomba uongozi
TFF.
Hivyo, amefungiwa miaka mitatu, adhabu ambayo itakwenda sambamba
na ile ya RUREFA ambapo kifungo chake sasa kitamalizika Oktoba 15, 2016.
Sekretarieti ya TFF imepewa onyo kali kwa kupokea fomu yake ya
kugombea na malipo wakati akiwa amefungiwa. Onyo hilo pia limetolewa kwa Chama
cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa Rukwa kwa kuidhinisha
fomu yake ya kugombea.
Naye Wilfred Kidao Mzigama ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
TFF amepatikana na kosa la kimaadili kwa kuwa na nyaraka la Kamati ya Utendaji
bila kibali na kukiuka taratibu za kuwasilisha malalamiko kwa mujibu wa Ibara
ya 12(2) na Ibara ya 50(1) na (5) ya Katiba ya TFF.
Amepigwa faini ya sh. milioni moja anayotakiwa kuilipa ndani ya
siku tatu ambapo akishindwa atafungiwa mwaka mmoja. Akitekeleza adhabu hiyo
ataweza kuendelea na mchakato wa kugombea uongozi kwa nafasi aliyoomba.
0 maoni:
Chapisha Maoni