Jumanne, 22 Oktoba 2013

LIGI KUU ENGLAND: JUMAMOSI NEWCASTLE KUFUNGUA NA LIVERPOOL





BAADAE JUMAMOSI VIGOGO MAN UNITED, ARSENAL, CHELSEA, CITY KILINGENI!!

RATIBA:

BPL: LIGI KUU ENGLAND
[Saa za Bongo]

MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 19 Oktoba
14:45 Newcastle United v Liverpool
17:00 Arsenal v Norwich City
17:00 Chelsea v Cardiff City
17:00 Everton v Hull City
17:00 Manchester United v Southampton
17:00 Stoke City v West Bromwich Albion
17:00 Swansea City v Sunderland
19:30 West Ham United v Manchester City
Jumapili 20 Oktoba
18:00 Aston Villa v Tottenham Hotspur
Jumatatu 21 Oktoba
22:00 Crystal Palace v Fulham







LIGI KUU ENGLAND inarudi tena dimbani baada ya kupotea kwa Wiki mbili kupisha Mechi za Kimataifa na itaanza Jumamosi kwa Mechi ya kwanza kabisa huko St James Park kati ya Newcastle na Liverpool.

IFUATAYO NI TATHMINI NA DONDOO FUPI ZA MECHI HIZO:
MECHI ZA JUMAMOSI
NEWCASTLE UNITED V LIVERPOOL
-St James’ Park

Hii ni Mechi ambayo jicho litakuwa kwa Daniel Sturridge wa Liverpool ambae Msimu huu ameshafunga Bao 6 katika Mechi 7 za Ligi na kwenye Mechi hii yupo kwenye mashambulizi pamoja na Straika hatari toka Uruguay, Luis Suarez.
Lakini nao Newcastle wanae Straika toka France ambae pia ni hatari, Loic Remy, aliefunga Bao 5 katika Mechi 3.

CHELSEA V CARDIFF CITY
-Stamford Bridge
Hii ni Mechi ambayo Kikosi cha Jose Mourinho kikiwa kwao Stamford Bridge kinategemewa kuibuka kidedea hasa kwa vile Meneja huyo Mreno ameamua kumrejesha kundini Juan Mata na pia kumchezesha Mbrazil Willian kwenye Kiungo.
EVERTON V HULL CITY
-Goodison Park
Mara ya mwisho Everton kucheza na Hull City Uwanja huu wa Goodison Park, Hull City walipigwa Bao 5.
Lakini safari hii, Hull City, chini ya Steve Bruce, hawajafungwa katika Mechi 4 huku Everton wakifungwa kwa mara ya kwanza Msimu huu walipocheza na Man City.
Everton, wakiwa na Romelu Lukaku, Ross Barkley na Steven Pienaar, ni hatari.

MANCHESTER UNITED V SOUTHAMPTON
-Old Trafford
Mabingwa Man United, baada ya kuchapwa kwenye Mechi mbili za Ligi mfululizo, walirudi kwenye ushindi kwa kuipiga Sunderland Bao 2-1 na Bao zote kufungwa na Chipukizi Adnan Januzaj.
Ni Mechi ambayo Mabingwa hao wa England hawapaswi kuipoteza ikiwa watataka kutetea Ubingwa wao.

STOKE CITY V WEST BROMWICH ALBION
-Britannia Stadium
Stoke City, chini ya Meneja Mark Hughes, wapo kipindi cha mpito cha kubadilisha staili yao toka lile Soka la miguvu kwenda Soka la kutandaza lakini wanapambana na West Brom Timu ambayo ipo kwenye moto ambayo haijafungwa katika Mechi 4 na imechapa Bao 7 katika Mechi hizo na Nyota wao kuwa Kijana Saido Berahino na Morgan Amalfitano.
SWANSEA CITY V SUNDERLAND
-Liberty Stadium
Baada kumtimua Paolo Di Canio, Sunderland sasa wana Meneja mpya Gus Poyet akihaha kuinasua Timu hiyo toka mkiani na safari hii wanapambana na Swansea ambayo imefungwa Mechi mbili mfululizo na Arsenal na Southampton licha ya kuwa na Mchezaji ‘Mpya kwa Timu ya Taifa ya Spain’, Michu.

ARSENAL V NORWICH CITY
-Emirates Stadium
Arsenal hawajafungwa katika Mechi 11 na wapo kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya Mechi 7.
Norwich walionyesha Soka safi walipocheza na Chelsea katika Mechi yao ya mwisho kabla kupigwa kwa Bao 2 za mwishoni.

WEST HAM UNITED V MANCHESTER CITY
-Upton Park
Baada ya West Ham kutua White Hart Lane na kuichapa Tottenham Bao 3-0  huku ‘Mtukutu’ Ravel Morrison kutoka Man United aking’ara na kufunga Bao lenye hadhi ya ‘Bao la Msimu’, ghafla Mechi hii imekuwa haitabiriki na hasa ikizingatiwa Man City hawajashinda Ugenini Msimu huu walipocheza na Aston Villa, Stoke na Cardiff na pia watatinga kwenye Mechi hii wakiikosa nguzo yao muhimu na Nahodha wao Vincent Kompany ambae ameumia.

MECHI YA JUMAPILI
ASTON VILLA V TOTTENHAM HOTSPUR
-Villa Park
Baada kuchapwa 3-0 Nyumbani kwao na West Ham, Tottenham watafarijika kusafiri na kutua Villa Park kucheza na Aston Villa Uwanja ambao hawajafungwa tangu Mwaka 2008 na Wiki kadhaa zilizopita walishinda Bao 4-0 kwenye Capital One Cup.
MECHI YA JUMATATU

CRYSTAL PALACE V FULHAM
-Selhurst Park
Crystal Palace wana Pointi 3 tu kwa Mechi 7 za Ligi lakini Fulham nao wako Nafasi ya 17 na wana Pointi 7.


MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
7
6
16
2
Liverpool
7
6
16
3
Chelsea
7
6
14
4
Southampton
7
5
14
5
Man City
7
9
13
6
Tottenham
7
4
13
7
Everton
7
1
12
8
Hull
7
-1
11
9
Man Utd
7
1
10
10
Aston Villa
7
1
10
11
Newcastle
7
-3
10
12
West Brom
7
1
9
13
West Ham
7
2
8
14
Cardiff
7
-2
8
15
Swansea
7
-3
7
16
Stoke
7
-3
7
17
Fulham
7
-4
7
18
Norwich
7
-4
7
19
Crystal Palace
7
-8
3
20
Sunderland
7
-11
1

Kutoa maoni



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top