HAMISI KIIZA 'DIEGO WA JANGWANI' BADO BAO MOJA TU KUMKAMATA TAMBWE SIMBA SC

HAMISI Friday Kiiza ‘Diego’ wa Yanga
SC leo hii amefikisha mabao saba katika mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0
dhidi ya Rhino
Rangers Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Hii inakuwa mechi ya pili mfululizo Mganda huyo anafunga mabao mawili kila mechi, baada ya Jumapili pia kufunga mara mbili katika sare ya 3-3 na wapinzani wa jadi, Simba SC Uwanja huo huo wa Taifa, Dar es Salaam.
Hii inakuwa mechi ya pili mfululizo Mganda huyo anafunga mabao mawili kila mechi, baada ya Jumapili pia kufunga mara mbili katika sare ya 3-3 na wapinzani wa jadi, Simba SC Uwanja huo huo wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes analingana na mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar ambaye pia ana mabao saba.
Wanaofuatia ni Elias Maguri wa Ruvu Shooting mwenye mabao sita, Themi Felix wa Kagera Sugar mwenye mabao matano sawa na Tumba Swedi wa Ashanti, wakati Didier
Kavumbangu wa Yanga SC ana ambao manne sawa na Kipre Tchetche Azam FC ambaye ndiye anashikilia tuzo ya ufungaji bora wa ligi hiyo
WANAOONGOZA KWA MABAO LIGI KUU:
JINA
TIMU MABAO
Amisi Tambwe Simba SC 8
Hamisi Kiiza Yanga SC 7
Juma Luizio Mtibwa 7
Elias Maguri Ruvu Shoot 6
Themi Felix Kagera 5
Tumba Swedi Ashanti 5
D. Kavumbangu Yanga SC 4
Kipre Tchetche Azam FC 4
Hamisi Kiiza Yanga SC 7
Juma Luizio Mtibwa 7
Elias Maguri Ruvu Shoot 6
Themi Felix Kagera 5
Tumba Swedi Ashanti 5
D. Kavumbangu Yanga SC 4
Kipre Tchetche Azam FC 4
0 maoni:
Chapisha Maoni