Jumapili, 13 Oktoba 2013


Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa kwa risasi iliyopigwa na mwanaume mmoja alieripotiwa kutokua na maelewano mazuri ambapo kwenye hili tukio mwanaume huyu alimpiga risasi na kumuua mama mzazi wa Ufoo Saro.

Mwanaume huyu alimpiga Ufoo risasi mbili ambazo zilimjeruhi na kudhani kwamba amemuua na kisha yeye mwenyewe kujipiga risasi na kufariki.

Mambo yote haya yalitokea huko Kibamba ambapo taarifa zisiso rasmi zinasema kwamba huyo mwanaume baada ya kuwa na ugomvi kati yake na Ufoo, alienda kuongea na mama mzazi wa Ufoo baada ya kuona mama yupo upande wa Ufoo ndio akaamua kuua.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top