Katika Mkutano wa
Kawaida wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 16 Januari 2013 Mwenyekiti kwa
niaba ya Kamati ya Utendaji aliwapa Wanachama wafikirie mapendekezo ya YANGA
kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa YANGA.
Nachukua nafasi hii
kuwaambia Wanachama wa YANGA kuwa kuanzia leo tarehe 16 Oktoba 2013 mpaka
tarehe 10 Novemba 2013, kutakuwa na sanduku moja (1) hapa Klabuni kwa ajili ya
kukusanya kura za maoni ya Wanachama ya kuanzisha Kampuni (NDIYO) au kutokuwa
Kampuni (HAPANA)
Kila Mwanachama hai
atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na Kadi yake ambapo
itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi.
Zoezi hili ni muhimu
kwa ajili ya maendeleo ya YANGA.
0 maoni:
Chapisha Maoni