CHEKI WALI HAO KTOKA BASERONA KISHA TAFAKALI MECHI KATI YA SIMA NA YANGA .
Tambwe: Nasikia tu Niyonzima
STRAIKA wa Simba, Amisi Tambwe amekiri kupata habari kwamba
kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima ni mtu hatari uwanjani lakini akadai hahofii
chochote.
“Kidogo nimesikia kuwa Niyonzima yupo vizuri lakini sijatazama
anavyocheza, pengine ningekuwa naangalia mechi za Yanga ningejua wachezaji wake
wakoje.”
“Kwa sasa hata nikitaka kuwajua, haitasaidia kitu kwa sababu
hao wana mipango yao na mimi nina mikakati yangu,” alisema Tambwe ambaye timu
yake inacheza na Yanga Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa Simba wanategemea kwamba Tambwe atawaokoa kwa
kukata ngebe za Yanga ambayo imekuwa ikitamba kwamba mastraika wake wana kasi
zaidi ya Simba.
Katika mechi tatu za Ligi Kuu za Simba zilizopita
Tambwe dhidi ya JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Prisons amepachika mabao mawili tu
kwa mikwaju ya penalti wakati mechi ya mwisho dhidi ya Prisons waliposhinda bao
moja hakufunga. Lakini amewaambia Simba wala hiyo isiwatishe
0 maoni:
Chapisha Maoni