Jumamosi, 20 Septemba 2014

WANAKIJIJI 700 WANYOA NDEVU,WENGINE 200 VIPARA KUOMBOLEZA KIFO CHA NYANI

WANAKIJIJI 700 WANYOA NDEVU,WENGINE 200 VIPARA   KUOMBOLEZA KIFO CHA NYANI

 Takriban wanakijiji 200 nchini India walinyoa nywele kama ishara ya kuomboleza kifo cha Nyani mmoja aliyekuwa akiishi karibu na hekalu lao.
Nyani huyo kwa jina Macaque, alizama alipoanguka kwenye bwawa la maji baada ya kufukuzwa na Mbwa.
Inaarifiwa watu hao waliamua kunyoa nywele ili kuepukana na laana.  
Waliandamana katika barabara wakiomboleza na kisha kumchoma Nyani huyo kuambatana na mila za kihindi.
Wanakijiji wengine 700 walinyoa ndevu zao.
Nyani huonekana kama mnyama mtakatifu kwa wahindi na kuna hekalu ambazo nyani anayejulikana kama mungu kwa wahindi Hanuman huabudiwa kote nchini India.

Alizama tarehe 2 Septemba na mwili wake ukatambuliwa na wanakijiji siku iliyofuata.Nyani huyo aliyefariki alikuwa mmoja wa Nyani wawili waliokuwa wanaishi karibu na hekalu katika kijiji cha Dakachya eneo la kati mwa India. 
''wazee wa kijiji walisema kuwa Nyani kufariki ndani ya kijiji sio jambo la kawaida. Tunahofia huenda ikawa bahati mbaya kwetu,'' alisema mmoja wa wazee wa kijiji bwana Patel.
"kwa hivyo tuliamua kumchoma Nyani huyo kuambatana na mila za kihindi kuhakikisha kuwa jambo baya halitatokea hapa kijijini. ''
Baada ya Nyani kuchomwa, wanakijiji walinyoa nywele na ndevu zao.
Wanakijiji wengine walichukua majivu ya Nyani huyo na kuyamwaga katika mto Ganges.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: WANAKIJIJI 700 WANYOA NDEVU,WENGINE 200 VIPARA KUOMBOLEZA KIFO CHA NYANI Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top