ROBINHO AREJESHWA KIKOSINI BRAZIL KUIVAA ARGENTINA
KOCHA
wa Brazil, Dunga amemuita tena kikosini mshambuliajo Robinho jana kwa
ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Argentina na Japan mwezi ujao.
Mshambuliaji
huyo aliachwa kwenye kikoi hicho cha Dunga mapema mwezi huu Brazil
ilipojipima nguvu na Colombia na Ecuador, lakini baadaye aliongezwa
kikosini kufuatia Hulk kuumia.
Brazil itacheza na Argentina Oktoba 11 huko Bird's Nest mjini Beijing na Japan siku tatu baadaye mjini Singapore.
Robinho alikuwa benchi Brazil ikiifunga Columbia 1-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Sun-Life
0 maoni:
Chapisha Maoni