Jumatatu, 3 Februari 2014

                Ivo Mapunda mkali balaa!

KIPA wa Simba, Ivo Mapunda amesisitiza ataendeleza ukali wake kwa wachezaji wote wa Simba anapokuwa uwanjani ili wazidi kuwa makini kiuchezaji.

Mapunda alisema: “Mimi huwa nina mikakati ninapokuwa uwanjani, nataka kuona wachezaji wenzangu wakiwa makini na kuendana na jinsi mpira unavyochezwa.

“Saa nyingine wanajisahau na ni haki yangu kuwakumbusha ingawa wanatafsiri kuwa mimi ni mkali lakini ina faida kwani mwishowe timu inapofungwa anayekuwa wa mwisho golini ni mimi,” alisema.
“Huwa nakua mkali kwa mabeki wangu nikitaka wawe makini zaidi kwenye mpira, pia wakati mwingine mazingira yakiwa magumu huwa nawakumbusha viungo na washambuliaji kuwa makini kwani wanaiweka timu hatarini kwa kiasi fulani wasipokuwa makini.

“Unajua mimi sipendi kufungwa mbali na timu yangu kupoteza mchezo, naamini kama kina Donald (Mosoti), Owino (Joseph), Kaze (Gilbert) na mabeki wengine wanakuwa makini basi kila mchezaji ataonekana bora na timu pia itaonekana bora.”

Mara kwa mara Mapunda amekuwa akiwakaripia wachezaji wenzake hususan wale wa nafasi za beki na kiungo huku wakati mwingine akiwasukuma akiwataka wakakabe hususan katika mipira ya kona na adhabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top