UGANDA YAWAFUNGA KENYA 1-0, SUDAN YAIFUMUA ERITREA 3-0
BAO
pekee la Dan Sserunkuma dakika ya 88, limeipa Uganda, The Cranes
ushindi wa 1-0 dhidi ya Rwanda, Amavubi katika mchezo wa Kundi C Kombe
la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge 2013 Uwanja wa
Nyayo, Nairobi jioni hii.
Rwanda
ilitawala sehemu kubwa ya mchezo na kukosa mabao mengi, lakini mwishoni
mwa mchezo ikawaruhusu Uganda kuondoka na pointi tatu
Wachezaji wote wa Yanga, Hamisi Kiiza alicheza upande wa Uganda na Haruna Niyonzima upande wa Rwanda.
Katika mchezo wa kwanza, Sudan iliifunga mabao 3-0 Eritrea kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Salah Ibrahim akifunga mawili na moja Tahir Mohammed
Baada ya kukamilisha mechi za kwanza za makundi, mechi za pili zitaanza kesho Ethiopia ikimenyana na Zanzibar na Sudan Kusini na Kenya, hiyo ikiwa michezo ya Kundi A Uwanja wa Nyayo.
Katika mechi za kwanza za kundi hilo, Zanzibar iliifunga Sudan Kusini 2-1 na Kenya ilitoka sare ya bila kufungana na Ethiopia.
0 maoni:
Chapisha Maoni