HABARI KUTOKA STANDARD RADI SINGIDA TANZANI
* Watu wanne
wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kwa kosa la unyang’anyi wa zaidi ya
shilling milioni nane kwa kutumia silaha
* Vyama vya siasa vilivyo na uwakilishi, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimewasilisha mapendekezo ya
kuboresha marekebisho ya Sheri ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.
* Shirika
la mpango wa chakula duniania WFP amesema kuna uwezekano wa kupunguzwa misaada
ya chakula inayopelekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na
kupungua fedha za taasisi hiyo.
* Jeshi la Nigeria limewaua wanamgambo 37 wanaodhaniwa
kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
HABARI KAMILI
Source;
Sr/Raymond/Operation
Ed;
Date; 23/10/2013
SINGIDA
Mkoa wa singida unatarajia kuanza operation ya ukaguzi wa kubaini watu
wanaoishi nchini kinyume na sheria.
Hayo yamebainishwa jana na Afisa uhamiaji mkoa wa Singida Bw. Adam
Mnyeke wakati akizungumza katika siku maalum ya polisi iliyofanyika katika
ukumbi wa Aquar Manispaa ya Singida,
Bw. Mnyeke amesema kuwa zoezi hilo linatarajia kuanza wiki ijayo, hivyo
kutoa wito kwa wananchi kuotoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ili kupambana na
wahamiaji haramu.
Amesema kwa kuanza, zoezi hilo litaanzia manispaa ya singida na baadaye
litakwenda katika wilaya nyingine za mkoa wa Singida, na kuongeza kuwa zoezi
hilo pia litasaidia kupambana na vitendo vya uhalifu ambavyo mara nyingi
vimekuwa vikifanywa na wahamiaji haramu.
Source; Sr/Chami/Mahakamani
Ed;
Date; 23/10/2013
SINGIDA
Watu wanne wamehukumiwa kifungo cha
miaka 30 Jela kwa kosa la unyang’anyi wa zaidi ya shilling milioni nane kwa
kutumia silaha
Akisoma hukumu hiyo hakimu mfawidhi
wa mahakama ya wilaya mkoani Singida Flora Ndale amesema tukio hilo limetokea
desember 8 waka 2012 katika barabara ya singida kwenda Dodoma maeno ya kisaki
Amesema siku ya tukio washtakiwa
waliweka mawe barabarani na kuteka gari lililokua likisafirisha maiti ya
mwanafuzi wa chuo kikuu cha Sokoine {SUA] kutoka morogoro kuelekea Tarime
Katika tukio hilo vitu mbalimbali
kama laptop, simu za mkononi, moderm mbili zote vikiwa na thamani ya shilingi
milioni nane laki saba viliibwa
Amewataja waliohukumiwa kuwa ni
Hamisi Issa, Halidi Hamisi, Abbubakari Jumanne, Hamisi Alli wote wakazi wa mkoa
wa Singida,ambapo siku ya tukio walikuwa na rungu,mawe na mashoka wakitumia
kufanya uhalifu huo
Hakimu Ndale amesema kitendo hicho
ni amesema adhabu hiyo itakua fundisho kwa watu wengine wanaofanya vitendo kama
hivyo.
Source;
Sr/Raymond/uhalifu
Ed;
Date; 23/10/2013
SINGIDA
Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa minne nchini iliyofanikiwa
kupambana na vitendo vya uhalifu kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha hivi
karibuni.
Mratibu wa Polisi kutoka makao
makuu Dar es salaam kitengo cha maadili James Kasusura amesema hayo wakati
akizungumza na washiriki wa kikao cha siku maalum ya polisi kilichofanyika
katika ukumbi wa Aquar manispaa ya Singida.
Kasusura ameyataja makosa yaliyopungua kuwa ni makosa dhidi ya
ubinadamu ambayo yamepungua kwa asilimia 35, makosa dhidi ya mali yamepungua
kwa asilimia 18, makosa dhidi ya maadili yamepungua kwa sailimia 13, na makosa
dhidi ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 12.
Amesema kupungua kwa makosa hayo kumetokana na ushirikiano baina ya
raia na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Singida, hivyo kutoa wito wa
kuendelezwa kwa ushirikiano huo na hatimae kukomesha vitendo hivyo kabisa.
Source;
Sr/Raymond/uhalifu
Ed;
Date; 23/10/2013
DAR ES SALAAM
Vyama vya siasa
vilivyo na uwakilishi, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na visivyokuwa na
uwakilishi bungeni vimewasilisha mapendekezo ya kuboresha marekebisho ya Sheri
ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.
Msemaji wa vyama
hivyo, ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw James Mbatia, amesema kuwa
mapendekezo hayo yalikabidhiwa kwa waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Miongoni mwa
waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na katibu mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod
Slaa, makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula, na mwenyekiti wa
CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Mbatia amesema kwamba wamekubaliana mapendekezo hayo yapelekwe katika mkutano
ujao wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo kwa hati ya dharura.
UNAENDELEA KUSOMA TAARIFA YA HABARI KUTOKA STANDARD RADIO NA SASA NI HABARI ZA KIMATAIFA.
Source: BBC Im( usalaama)
Source: BBC Im( usalaama)
Ed
Date: Wednesday October 23, 2013
KINSHASA
Shirika
la mpango wa chakula duniania WFP amesema kuna uwezekano wa kupunguzwa misaada
ya chakula inayopelekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na
kupungua fedha za taasisi hiyo.
Msemaji wa
taasisi hiyo amesisitiza kuwa, shirika hilo limepokea asilimia 50 tu ya fedha
inazohitajia kwa ajili ya kusaidia chakula katika kipindi cha miezi 6 ijayo.
Aidha
amesema mpango wa Chakula Duniani unakabiliwa na upungufu wa dola milioni 70 hivyo unalazimika kupunguza misaada kuanzia
mwezi november
Upungufu huo wa misaada ya chakula utawaathiri karibu wakimbizi laki 3
wanaohitajia misaada ya chakula katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa
Kongo. Asilimia 60 ya familia za mkoa huo zinakabiliwa na uhaba wa chakula
Source: BBC Im( usalaama)
Ed
Date: Wednesday October 23, 2013
JUBA
Raia 856
wa Sudan Kusini waliokuwa wakiishi Sudan wamewasili mjini Juba baada ya
kusafiri kwa siku 17 kwa kutumia jahazi
Kwa miaka
kadhaa sasa mpango wa wananchi hao kurejea Sudan Kusini ulikuwa unakwama kwenye
mpaka wa kaskazini katika eneo la Renk
Msemaji wa
shirika la IOM Bw Jumbe Omari Jumbe
amesema kupitia mpango wa usaidizi wa kurejea nyumbani uitwao OTA, IOM kuanzia
mwaka huu imesaidia watu elfu sita
wa sudan kusini kurejea kwao
Amesema
zoezi la utambuzi lililofanyika katikati ya mwaka huu huko Renk lilibaini
kuwepo kwa watu Elfu Tatu waliokwama eneo hilo wakisubiri kuelekea Sudan
Kusini.
Source: BBC Im (vifo)
Ed
Date: Wednesday October 23, 2013
ABUJAJeshi la Nigeria limewaua wanamgambo 37 wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa jeshi la Nigeria katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo Kapteni Aliyu Danja amesema jeshi lilifanya mashambulizi dhidi ya kambi ya Boko Haram huko Alagano.
Kapteni Danja ameongeza kuwa oparesheni hiyo iliyoanza juzi Jumatatu ilihusisha mashambulizi ya nchi kavu na angani kwa lengo la kuisambaratisha ngome ya wanamgambo wa Boko Haram huko Alagano.
Mwezi Mei 15 mwaka huu jeshi la Nigeria lilianzisha mashambulizi dhidi ya kundi la Boko Haram siku moja baada ya Rais Goodluck Jonathan kutangaza hali ya hatari kwenye majimbo matatu ya Borno, Yobe na Adamawa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo
Kabla ya kumaliza kusoma taarifa ya habari huu tena ni muhtasari wake
* Watu wanne wamehukumiwa kifungo
cha miaka 30 Jela kwa kosa la unyanganyi wa zaidi ya shilling milioni nane kwa
kutumia silaha
* Vyama vya siasa vilivyo na uwakilishi, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimewasilisha mapendekezo ya
kuboresha marekebisho ya Sheri ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.
*
Shirika la mpango wa chakula duniania WFP amesema kuna uwezekano wa kupunguzwa
misaada ya chakula inayopelekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
kutokana na kupungua fedha za taasisi hiyo.
* Na Jeshi la Nigeria
limewaua wanamgambo 37 wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram huko
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Na
huo ndio mwisho wa taarifa ya habari kutoka standard redio
0 maoni:
Chapisha Maoni